Umoja wa Mataifa umeitaka China kuheshimu haki za binaadamu za watu wa jamii ya Uighur.

Wito huo wa pamoja umetolewa na nchi takriban 40 katika mkutano kuhusu haki za binaadamu Balozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa, Christoph Heusgen amesema wanaitaka China kuheshimu haki za binaadamu hasa za makabila ya watu wachache pamoja na dini, kwenye majimbo ya Xinjiang na Tibet.

Miongoni mwa nchi 38 zilizosaini wito huo ni pamoja na Marekani na nchi nyingi za Umoja wa Ulaya ikiwemo Albania na Bosnia, pamoja na Canada, Haiti, Hondurus, Japan, Australia na New Zealand. Nchi hizo pia zimeelezea wasiwasi wao kuhusu hali ya Hong Kong.

Hata hivyo, balozi wa Pakistan amesimama na kusoma taarifa iliyosainiwa na nchi 55 ikiwemo China, inayolaani kile inachokiita ‘unafiki’ wa nchi zinazoitumia hali ya Hong Kong kama kisingizio cha kuingilia masuala ya ndani ya China.

Kocha KMC ajitetea vichapo VPL
Vyama viwili vyajitoa kumuunga mkono JPM