Ni utamaduni wa wasanii wengi hasa Chipukizi kukusanya kitita cha pesa na ‘kuwahonga’ watangazaji wa redio ili wapige nyimbo zao, kwa kuibariki hongo hiyo kwa jina la ‘promo’. Lakini B12 akiipokea fedha ya msanii husika, itakula kwake!

Mtangazaji huyo wa kipindi maarufu cha XXL, amesewatahadharisha wasanii wanaotaka kutumi fedha zao kumhonga ili acheze nyimbo zao hakuna cha maana watakachopata kama ‘promo wanayoiota’.

“It’s true kuna watu wanakuja na hela kabisa wanakwambia mimi nina kiasi kadhaa nataka unifanyie promotion. Lakini ukweli haupo hivyo. Unajua unaponipa mimi hela yako ili nipige nyimbo yako, nitaipiga siku mbili halafu nitaipotezea,” B 12 aliiambia Mkasi TV.

Alieleza kuwa kama wangekuwa wanapiga nyimbo za wasanii kutokana na namna ambavyo msanii husika anatoa pesa, kipindi chao kisingeweza kuwa kipindi cha burudani kinachoongoza nchini.

 

Aliwashauri wasanii kuwa makini wanapofikiria kutumia fedha kusambaza kazi zao kwa kuwa kiuhalisia muziki kweli unahitaji fedha kwa kuwa ni biashara kama zilivyo biashara nyingine.

Msafara wa Magufuli wasimamishwa Morogoro, Awanyooshea kidole hawa
Ali Kiba: Usinifananishe na Msanii yeyote Tanzania