Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi, jana usiku walivamia na kuwaua kwa kuwachinja watu wanane katika kitongoji cha Kibatini kata ya Mzizima, Wilaya ya Tanga na kisha kuiba vyakula.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Leonard Paul

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Leonard Paul

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Leonard Paul amesema kuwa tukio hilo la kikatili lilitokea majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo, umbali wa Kilometa 45 kutoka Tanga Mjini.

Amesema kuwa watu hao walivamia nyumba tatu katika eneo hilo lenye nyumba 20 baada ya kuvuka msitu unapotokea Tanga Mjini, wakiwa na visu mapanga. Baada ya kutekeleza mauaji hayo, watu hao waliiba sukari, biskuti na mchele kabla ya kutokomea kwenye msitu ulio karibu na mapango ya Amboni.

Kamanda Paul alisema kuwa Jeshi la Polisi linashirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanawatia nguvuni watu hao ili sheria ichukue mkondo wake.

Magufuli: Ni Tanzania Pekee ukifeli kidato cha nne unajiunga Chuo Kikuu!
Wauaji wa Albino washughulikiwe sasa.....