Msichana mmoja ameeleza mkasa wa kusikitisha wa maisha ya kufanyiwa unyama na wanaume waliombaka zaidi ya mara 43,000 baada ya kushikiliwa kama mateka katika biashara ya binadamu nchini Mexico.

Karla Jacinto ameeiambia CNN kuwa anakadiria kuwa alibakwa mara 43,2000 katika kipindi chote alichoshikiliwa na mfanyabiashara huyo haramu kwa kuwa alikuwa akilazimishwa kufanya mapenzi na wanaume zaidi ya 30 kwa siku ndani ya miaka minne.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 alieleza kuwa mara ya kwanza alikamatwa akiwa na umri wa miaka 12 na mfanyabiashara huyo haramu aliyemrubuni na kumtenganisha na familia yake kwa kutumia zawadi mbalimbali.

Karla-Jacinto2

Alieleza kuwa alipelkwa katika jiji la Guadalajara nchini Mexico na kulazimishwa kufanya kazi ya kujiuza.

Alieza pia mateso aliyopewa na mfanyabiashara huyo alipokuwa akimlazimisha kufanya ngono na watu asiowafahamu.

“Nilianza kufanya mapenzi kuanzia saa nne asubuhi hadi usiku wa manane. Wanaume wengine walikuwa wakinicheka. Ilinibidi nifumbe macho ili nisiweze kuona wanachonifanyia ili nisihisi chochote. Alinipiga makonde, alinipiga mateke na kuvuta nywele zangu, alinitemea mate usoni… na wakati mwingine alinichoma na pasi,” msichana huyo alieleza CNN mkasa huo wa kusikitisha.

Aliokolewa katika operesheni maalum ya jijini Mexico iliyolenga katika kukomesha biashara ya binadamu nchini humo.

Hivi sasa amejiunga na harakati za kuzuia biashara ya binadamu nchini humo. Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la uhamiaji, zaidi ya wanawake 20,000 wanasadikika kuathiriwa na biashara hiyo haramu na ya kikatili kila mwaka.

 

Raia Wa Liberia Aondolewa Kwenye Kinyang'anyiro
Mvua Yaahirisha Uhondo Wa Soka Buenos Aires