Uongozi unaomsimamia Mshambuliaji kutoka DR Congo Jean Baleke umeweka wazi kuwa umepokea ofa kutoka kwa timu nyingi zikiwemo zinazocheza katika ligi mbalimbali barani Ulaya.

Jean Baleke ambaye anakipiga katika klabu ya Simba SC kwa mkopo akitokea TP Mazembe amekuwa akifanya vyema ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi, kwani tangu atue klabuni hapo mwezi Januari 2023 amefunga mabao nane katika mechi nane alizocheza kwenye ligi jambo ambalo mashabiki wengi wamekubali uwezo wake.

Meneja wa Mshambuliaji huyo Faustino Mkandila ameweka wazi kuwa juu ya timu kutoka Ulaya zikiwa zinamhitaji mchezaji huyo kupitia dirisha kubwa jambo ambalo lazima Simba SC wafanye kazi kubwa kumbakisha mshambuliaji huyo.

“Baleke yupo Simba SC kwa mkopo hivyo viongozi wa klabu hiyo wanatakiwa kufanya kazi kubwa sana kumbakisha Baleke kutokana na timu nyingi kumnyatia haswa kutoka Afrika na Ulaya.

“Tayari timu nyingi zimeleta ofa ya kumuhitaji Baleke hadi timu kutoka ligi za Ulaya wameonekana kuvutiwa na uwezo ambao ameuonyesha hivyo kuna kazi kubwa lazima itumike kwa Simba SC kama watahitaji kuendelea kuwa na Baleke kutokana na uwezo mkubwa alionao,” amesema kiongozi huyo

Hamasisheni matumizi Takwimu za Sensa kiuchumi - Othman
Bosi Young Africans afichua siri usajili wa Chivaviro