Meneja wa Diamond Platinumz, Babutale amesema hali ya Hawa wa Nitarejea inaendelea vizuri na madaktari wamehakikisha kuwa atakuwa salama mara baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa uliohitaji uangalizi wa hali ya juu.

Amesema tumbo la Hawa limeanza kupungua na Mungu akijaalia baada ya wiki moja na nusu ataanza safari ya kurejea nchini Tanzania.

”Asante Mungu amemaliza salama ivi amesha zinduka na madaktari wametupa uhakika wa mgonjwa atakua salam na mpaka ivi sasa tumbo limeshaanza kupungua na Mungu akipenda baada ya wiki moja na nusu ataruhusiwa kurudi Dar”.

Hawa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu na tumbo kujaa maji ambapo madaktari nchini walisema kuwa anatatizo la ini hali ambayo imekuwa tofauti alipofanyiwa uchunguzi wa kina nchini India na kugundulika na tatizo la moyo lililosababisha sehemu hizo za mwili wake kujaa maji.

Shukrani za dhati kabisa ziwaendee uongozi mzima wa WCB kwa kulisimamia jambo hili na kulifanikisha na kuokoa maisha ya msanii Hawa.

Aidha kabla ya kwenda India Hawa alihojiwa na chombo cha habari cha Dar 24 ambapo alisema Mungu akimjalia uzima ataendelea na kazi yake ya muziki hivyo watanzania wamuombee arejee salama.

Trump, Putin kuteta jijini Paris
Wanakijiji waomba serikali iwapelekee mganga wa jadi