Klabu za Soka Barani Ulaya zinaendelea kupigana vikumbo katika harakazi za kuwania saini za wachezaji kwenye kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa 2021/22.

Tetesi za usajili zimeshika hatamu, huku klabu nyingine zikifanya kweli kwa kusajili wachezaji ghali na kujipanga kuwatangaza hadharani kupitia vyombo vya habari.

Hizi ni baadhi ya taarifa za usajili ambazo zimechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari Barani Ulaya kuamkia leo Jumatatu (Julai 05).

~Junior Firpo (Hispania) atatangazwa rasmi kama mchezaji mpya wa Leeds United kesho. Barca watapokea kiasi cha €15M na atasaini mkataba wa miaka minne ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Marcelo Bielsa.

~Sergio Ramos (Hispania), Achraf Hakimi (Morocco) na Gianluigi Donnarumma (Italia) watatangazwa kama wachezaji wapya PSG, Mipango ya vipimo vya afya kwa ajili ya Ramos imeshaandaliwa, atasaini Mkataba mpaka June 2023. Hakimi mpaka 2026, Wakati Donnarumma atasaini mpaka June 2026.

~PSG imeanza mazungumzo kuhusu kumsajili Paul Pogba kutoka Manchester United, wakati huo tayari imemuwasilishia kiungo huyo Mfaransa azma ya kuchukua mataji mbeleni

~Rasmi na imethibitishwa
Cengiz Ünder anajiunga na Olympique Marseille akitokea AS Roma. Pau López and Matheo Guendouzi watafuatia, wakati William Saliba naye yupo mwishoni kusajiliwa klabuni hapo.

Gomes: Nipo tayari kuwajibika kama kocha
Masau Bwire aionya Young Africans