Kuwa na Ndevu au nywele za usoni ni jambo zuri, na asilimia kubwa ya vijana wadogo wa kiume huwa na ndoto ya kuzipata ili waone muonekano wao wa kiutu uzima utakuwaje.
Lakini wanapokuwa, na ndevu zikachomoza, wanazipunguza na baadhi yao huziondoa kabisa kwani wanagundua haziwafanyi kuwa huru kama walivyo fikiria mwanzo.
Haijalishi na kwasababu zipi, inaweza kuwa ni kufuata mitindo ya wakati (Fashion), au kufuata sheria za dini, jambo la muhimu la kulifahamu ni kuwa kufuga ndevu kunafaida kiafya, leo utafahamu mambo matano ambayo yanaweza kukusahangaza juu ya Ndevu.
- Nikinga dhidi ya Bakteria na Maambukizi
Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka 2015 tafiti zilipotoka juu ya uwezekano wa ndevu kubeba bakteria na vijidudu zilizua taharuki na kupelekea jopo la madaktari kutoka ulaya kufanya tena utafiti kwa wanaume takribani 408.
wanaume wenye ndevu na wale wasio na ndevu wote walifanyiwa utafiti na kubani kuwa wale wasio na ndevu walikuwa na hatari ya kubeba vijidudu bakteria mara tatu zaidi ya wale wenye ndevu.
Hivyo basi ufugaji wa ndevu umeonekana kutoa kinga dhidi ya vijidudu endapo zitawekwa kwenye hali ya usafi wakati wote.
2 . Hukinga uso dhidi ya mwanga wa jua
Ni ukweli usio pingika kuwa mwanga wa jua una umuhimu mkubwa sana kwenye ngozi ya binadamu lakini ukizidi ni hatari, kwani huweka ngozi kwenye hatari ya kupata kansa kutokana na mionzi ya ‘Ultraviolet rays’.
Endapo mwanaume atakuwa na nywele za usoni (Ndevu), anaweza kujikinga na mwanga huo kwa asilimia 90 hadi 95, japokuwa inategemeana na urefu wa ndevu na upande wa jua unavyopiga.
3. Hukua mara nne zaidi ya kimo cha binadamu
Imeelezwa kuwa makadirio ya ukuaji wa ndevu, asilimia 55 ya wanaume wote duniani, wanaofuga za chini ya mdomo au za juu ni inchi 5 na nusu kwa mwaka hivyo basi endapo mwanaume hata nyoa hata maramoja ndevu zake anaweza kufariki akiwa na ndevu ndefu zenye urefu wa miguu 27 na nusu ya binadamu.
4. Ndevu kwa wanawake hurefuka pia.
Kwamujibu wa rekodi za Guinness, binadamu aliyewahi kuwa na ndevu ndefu zaidi duniani ni Hans Langseth mwanaume aliyefariki 1927 akiwa na ndevu zenye urefu wa miguu 17.
Lakini kwa upande wa mwanamke anayeshikiria rekodi ya kuwa na ndevu ndefu zaidi duniani ni Vivian Wheeler kutokea Wood River iii, ambaye aliamua kufuga ndevu zake baada ya kifo cha mama yake na baada ya ndoa zake nne kuvunjika, alikufa mwaka 1993 akiwa na ndevu zenye urefu wa inchi 10.04.
5.Huongeza hali ya kujiamini.
Inaelezwa kuwa watu ambao wanaugojwa wa kuogopa ‘pogonophobia’ pia hujikuta wanaogopa ndevu.
Hivyo basi tafiti zimebaini kuwa watu wengi wanaofuga ndevu hujiamini katika kufanya maamuzi yao hasa kwenye kundi la watu licha ya kuwa muonekano wao pia huchangia watu kuwaona watofauti na wanamawazo yamuhimu.
Hayo ni mambo machache ambayo wengi wamekuwa hawayafahamu juu ya ukweli kuhusu ufugaji wa ndevu, endelea kutembelea ukarasa huu kufahamu mambo mbalimbali.