Vigogo 12 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayoongozwa na Rais Ali Mohamed Shein, wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za kuhusika katika kula njama na kusababisha upotevu wa kiasi kikubwa cha fedha za umma.

Waziri wa Fedha na Mipango wa SMZ , Dk. Khalid Salum Mohamed aliwaambia waandishi wa habari kuwa kati ya waliosimamishwa kazi ni pamoja na Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali na wahasibu wakuu wa wizara sita.

Alisema kuwa uchunguzi uliofanyika ulibaini kuwa upotevu huo wa fedha ni wakupangwa na umetekelezwa kwa uhusika wa watendaji wa idara na vitengo vya fedha serikalini.

Waziri huyo wa Fedha na Mipango alisema kuwa kutokana na vitendo hivyo viovu, hundi ya shilingi milioni 517 imeshindwa kulipwa. Alisema uchunguzi unaendelea kubaini wahusika zaidi na kwamba kuna uwezekano kiasi cha fedha kilichopotea kikawa kikubwa zaidi.

Hii ni idadi kubwa zaidi ya vigogo wa ngazi za juu katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika awamu hii kutumbuliwa jipu.

Wananchi waichongea Clouds TV kwa TCRA kwa kurusha 'mada ya ushoga', Makonda awakingia kifua
Video: Rais Magufuli amewaapisha wakuu wanne wapya wa mikoa