Afarah Suleiman, Hanang – Manyara.
Mkuu wa wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja amezindua jengo la kujifungulia kina mama katika kata ya Dumbeta, Wilayani humo na kuwataka Wananchi kutunza miundombinu ya jengo hilo na Zahanati kwa ujumla.
Akiwa Katia uzinduzi huo, DC Mayanja amewakaribisha wadau wa maendeleo kujitokeza kufanya maendeleo, ili kuipa sapoti Serikali na kuwasaidia Wananchi Wilayani humo.
Naye mganga mfawidhi wa Zahanati hiyo, Meshaki Mesai alisema kabla ya jengo Hilo kujengwa iliwalazimu kutoa rufaa kwa akina mama, ambazo hazikuwa na ulazima au sababu za kitabibu ila kutokana na changamoto Hiyo ya kukosa jengo la kujifungulia iliwalazimu kufanya hivyo.
Nao baadhibya Wananchi wa Dumbeta wameishukuru serikali pamoja Na wadau wa maendeleo kutatua kero kubwa iliyokuwa inawakabili kina mama ya kukosa wodi yakujifungulia wakati wa mimba hadi kupelekea kina mama wengi kupoteza watoto kutokana na kufata huduma mbali.
Kata ya Dumbeta, ipo Wilayani Hanang’ ikiwa na Vijiji tisa na Wananchi 9,421 ambapo wote kwa pamoja watanufaika na Zahanati hiyo.