Uongozi wa Manchester United, umemtaka meneja wa sasa Louis van Gaal kuendelea kusalia klabuni hapo kama mkurugenzi wa soka, ili kupisha ujio wa Jose Mourinho katika benchi la ufundi.

Van Gaal, ametakiwa kubadili upepo wa uongozi wake klabuni hapo, kwa kupewa jukumu zima la kusimamia masuala yote ya soka sambamba na kubaki kama mshauri wa benchi la ufundi, ambalo huenda likaendeshwa na Mourinho kama mipango itakwenda vyema.

Anayefanya kazi ya ushauri huo kwa Van Gaal, ni mtendaji mkuu wa Man Utd, Ed Woodward na anaamini hakuna jambo lolote litakalo badilika kama watafikia makubaliano na meneja huyo kutoka nchini Uholanzi.

Hata hivyo Van Gaal ambaye tayari ameshatumikia miaka miaka miwili katika mkataba wake wenye muda wa miaka mitatu, bado hajatoa jibu kamili la kukubaliana na mpango huo mpya.

Lakini pamoja na kuwepo kwa kigugumizi cha kutolewa kwa majibu, tayari Woodward ameshawahakikishia wajumbe wa bodi ya Man Utd, juu ya jambo hilo kuwezekana kwa asilkimia zote, ili kupisha utawala mpya wa benchi la ufundi chini ya Mourinho.

Meneja huyo kutoka nchini Ureno, ambaye ameshawahi kuzinoa klabu za FC Porto, Chelsea, Inter Milan pamoja na Real Madrid, ameshakataa ofa kadhaa zilizolengwa kwake, kwa kuamini ana kila sababu ya kutajwa kama mkuu wa benchi la ufundi huko Old Trafford.

Enner Valencia Kuwarithi Victor Anichebe, Stephane Sessegnon
Diamond atajwa kati ya wanaowania tuzo za BET 2016