Aliyekua mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi, Robin van Persie amesema aliwahi kupigwa kofi zito na kocha wa zamani wa kikosi cha The Orange, Louis van Gaal wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2014.

Mshambuliaji huyo aliyewahi kuzitumikia Arsenal na Manchester United za England, amesema tukio hilo lilitokea wakati wa mchezo hatua ya robo fainali, kati ya Uholanzi dhidi ya Costa Rica, na mchezo ulimalizika kwa sare ya 0-0.

Van Persie amesema wakati wa dakika 30 za nyongeza (Extra Time) alipatwa na maumivu ya misuli, na Van Gaal alitaka kumtoa, lakini mshambuliaji huyo alikataa.

“Mchezo ulienda kwenye dakika za nyongeza na nikapata maumivu, Louis alipiga kelele “Ninakutoa”. Niligeuka na kumjibu “hapana, hapana, tuna penati zinafata” lakini nakumbuka zile dakika 20 za mwisho zilikuwa ngumu sana kwangu kutokana na majeraha.”

“Yeye (Van Gaal) aliweza kuona hilo tatizo na alikuwa amekasirika sana” Mechi ilipomalizika na tukakusanyika karibu, alinikaribia na ghafla akanichapa..Paah kofi zito! Kwa kiganja chake kikubwa alinipiga kofi na akasema kwa hasira “usinifanyie hivyo tena”.

“Nilimwangalia kwa mshangao kabisa. Louis alisema ” hakikisha unaweka mpira kwenye wavu mara moja”.

“Kwa bahati nzuri niliweza kufunga ile penati. Ninapofikiria tena juu ya tukio hilo, ulikuwa wakati mgumu, lakini huyo ndio Van Gaal. ”

Uholanzi ilishinda kwa penati lakini kisha waliondoshwa na Argentina katika hatua ya Nusu fainali.

Maofisa wawili TRA watiwa mbaroni kwa kuomba rushwa
Wafahamu kidogo Ihefu Sports Club