Tuzo za Nzumari ambazo ni moja kati ya tuzo maarufu nchini Kenya zilitolewa mwishoni wa juma lililopita huko Mombasa nchini humo na kuwatuza Ali Kiba na Vanessa.

Katika tuzo hizo, Ali Kiba aliibuka mshindi wa tuzo ya ‘Msanii Bora wa Kiume kutoka Tanzania’ akiwashinda, Shetta, Ommy Dimpoz, AY na Rich Mavoko waliokuwa wametajwa kwenye kipengele hicho.

Naye mkali wa ‘Never Never’, Vanessa Mdee alitajwa kuwa mshindi wa tuzo ya msanii bora wa kike kutoka Tanzania akiwashinda Lady Jay Dee, Shilole, Shaa na Linah.

Tuzo hizo zilitolewa kutoka na kura zilizopigwa na waliopata kura nyingi ndio waliotajwa kuwa washindi.

Going Bongo Yabamba, Ni Filamu Pekee Ya Bongo Inayooneshwa kwenye Jumba la ‘Cinemax Centuries’
Himid Mao Azungumza Kilichowaponza Dhidi Ya Simba