Mwanamuziki mkubwa mwenye mashabiki wengi Afrika kwa sasa, Vannesa Mdee ‘Vee Money’ au  Cash Madame amepata shavu la kuuza sura katika msimu wa tano wa Tamthilia ya MTV iitwayo MTV Shuga, ambapo msimu uliopita mwadada Lupita Nyongo mwenye asili ya kenya alitikisa na kufanya vizuri katika Tamthilia hiyo.
Vee Money amefanya mahojiano na Uwazi Showbiz, ameleza kwa upana umahiri wake na jinsi alivyopata  kazi hiyo mpya iliyompa shavu na kuuza sura kwenye tamthlia hiyo.

Vanessa ameeleza ” Nilipata kazi kwa kufanya ‘audition’ baada ya wao wenyewe kuniomba nifanye hivyo”.

Ambapo Vee Money aliweza kuelezea changamoto alizokutana nazo katika kutengeneza Tamthilia hiyo, ilihali hajawahi kufanya maigizo karibuni kwani amekuwa akijikita zaidi katika muziki.

”Kumeza script ni kazi ngumu lakini kwa kuwa nimeamua kufanya, inabidi kukomaa” amesema Vanessa.
Pamoja na changamoto hiyo, kubwa kuliko zote Vanessa ameeleza ni pale ambapo alitakiwa kuvaa uhusika ambao haendani nao, lakini ilimbidi kufanya kazi kwa juhudi ili kutendea haki uhusika huo na pia kutowaangusha wale waliomuomba kuigiza kwani waliamini anaweza na hana budi kufanya hivyo ili kuwahahakikishia kweli anaweza kazi ya sanaa.
Vanessa alitoa shukrani za dhati kwa Mungu na uongozi mzima wa Tamthilia ya MTV Shuga kwani kuigiza ni moja ya ndoto zake, kupitia kazi hiyo aliahidi kuitumia kama mlango wa kutokea kufanya kazi nyingine nyingi za maigizo.

 

CCM haimuachii Lowassa, Polepole aanza nae...
Video: Maiti iliyozikwa Mbeya yakutwa nyumbani, Mbowe ataja kinachowaliza