Mwanamitindo na mfanyabiashara, Victoria Beckham jana alihudhuria tuzo za Glamour zilizotolewa jijini New York Marekani ambapo alishinda tuzo ya ‘Women of the Year’ na kuonesha mapenzi yake kwa mumewe, David Beckham.

Akipokea tuzo hiyo jukwaani, Victoria alielezea jinsi anavyompenda mumewe na mchango wake katika maisha yake.

Victoria Beckham

“Kuendesha bishara zangu, kazi yangu na UNAIDS na muhimu zaidi kuwa mama isingewezekana bila David. Sio tu kwamba ni baba wa kipekee, lakini pia ananisapoti na ni mtu anayenipenda na kunivutia kila siku,” alisema Victoria.

Katika hotuba yake hiyo iliyovuta usikivu wa watu wengi waliomshangilia, aliwahamasisha wanawake wenzake kuzifanyia kazi ndoto zao ili waweze kufanikiwa.

“Mimi kusimama hapa usiku huu kupokea tuzo hii inathibitisha kuwa kama una ndoto kubwa na unafanya kazi kwa bidii, hakuna kikwazo ka kile unachoweza kufanikisha.”

Stewart Hall: Malengo yetu ni robo fainali Afrika
IAAF Yaitega Urusi Hadi Juma Lijalo