Kampuni ya DataVision International ya Jijini Dar es salaam inayojishughulisha na masuala ya utafiti wa mambo mabali mbali, imetoa mafunzo ya siku nne kwa watathmini ambao watatembelea mashule kwa ajili ya kupata takwimu ambazo zitaisaidia Serikali na wadau wa elimu nchini kutatua matatizo yanayoikumba sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Mshauri Elekezi wa Kampuni hiyo, Macmillan George alipokuwa akifunga mafunzo hayo, amesema kuwa, mafunzo hayo yamelenga kuisaidia Serikali katika kutatua matatizo mbalimbali ya katika sekta ya Elimu.

“Mafunzo haya yamechukua muda mrefu kidogo, lakini yalikuwa na lengo zuri la kuhakikisha watathmini wanaelewa kile wanachoenda kukifanya,”amesema Macmillan.

Video: 'Hatujihusishi na uhalifu' - Waendesha Boda boda
Magazeti ya Tanzania leo Machi 26, 2017