Waendesha Boda Boda wamekuwa wakitajwa kuhusika katika matukio mbali mbali yakiwemo ya uhalifu, kusababisha ajali kutokana na uzembe na kutokuzingatia sheria za barabarani.

SAUTI ZETU ya Dar24 imezungumza na waendesha boda boda hao katika jiji la Dar es salaam, ambapo wameeleza mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuhusu tuhuma za uhalifu zinazoelekezwa kwao, wamesema kuwa tuhuma hizo si za kweli kwani wao ni watu wenye weledi katika kazi yao.

Wamesema kuwa kazi ya kuendesha boda boda ni kazi kama kazi nyingine na inapaswa kuheshimiwa.

“Sisi boda boda hatujihusishi na masuala ya uhalifu lakini kuna baadhi ya watu ambao hawafanyi kazi hii lakini wa boda boda kwaajili ya kufanyia uhalifu,”amesema mmoja wao.

Video: Rungu la JPM laibua Kontena zingine..., Prof. Lipumba aendelea kumkomalia Maalim Seif
Video: DataVision International kupeleka watafiti wa elimu mashuleni