Video inayomuonesha Simba jike akipambana na kusombwa na mafuriko yanayotokana na mvua za masika zilizoanza hivi karibuni imepata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii na kuzua maswali.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache baada ya Simba kuonekana katikati ya jiji la Nairobi na kumjeruhi mtu mmoja kabla hajalazimishwa kurudi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Nairobi.

Simba huyo alionekana kusombwa na maji na kutokomea, ingawa tovui ya Kenyans ilimkariri mtu mmoja akieleza kuwa alimuona Simba huyo akijiokoa kutoka kuingia kwenye maporomoko baada ya kujiokoa kuzama.

Mkuu wa kitengo cha ‘Veterinary Services’, Dk. Francis Gakuya alieleza kuwa timu yake haikuweza kumfikia Simba huyo kwa muda baada ya kukwama kwenye tope umbali wa Kilomita 3.

Kundi la kigaidi la ISIS laibukia Afrika Mashariki
Nape ashusha rungu kwa uongozi wa Yanga