Mwezi uliopita, Tasnia ya muziki wa Bongo Flava ilikosa furaha iliyokuwa ikiitarajia baada ya kutoka mikono mitupu kwenye tuzo za MTV MAMAs (2016), zilizofanyika Johannesburg, Afrika Kusini.

Mtangazaji wa The Playlist ya 100.5, Times Fm, Omary ‘Lil Ommy’ Tambwe, alihudhuria tukio hilo na alikuwepo Johannesburg wiki moja kabla ya tuzo na siku kadhaa pia baada ya tukio hilo akikusanya ‘data’.

Alifanya mahojiano na wasanii, waandaaji wa tuzo pamoja na watu maarufu walioshiriki katika utoaji wa tuzo hizo, na jicho lake liliona mengi na masikio kusikia mengi yatakayokusaidia kutegua kitandawili cha kilichojiri katika tuzo hizo.

‘Lil Ommy’ amefunguka katika mahojiano maalum na Dar24 kuhusu joto la tuzo hizo, kama tulionewa, walichokisema waandaaji wa tuzo hizo, mpango wa kuzileta Dar es Salaam, na mengine mengi usiopaswa kuyakosa.

Kwa mara ya kwanza, wasanii wengi zaidi wa Tanzania walitajwa kuwania tuzo katika vipengele mbalimbali lakini matokeo hayakuwa mazuri.

Angalia hapa:

 

Maafande Wa Ruvu Shooting Wagomea Mchezo Ligi Kuu
Mario Balotelli: Ni Wakati Wa Luis Suarez