Mtandao wa biashara ya mtandaoni Jumia Mobile, unatarajiwa kuanza Mei 22 na kumalizika Mei 28 mwaka huu ambapo utakuwa maalumu kwa ajili ya mauzo ya simu na vifaa vyake kutoka makampuni mbalimbali Tanzania yanayoshirikiana na JUMIA.

Aidha, katika wiki hilo la JUMIA kutakuwa na punguzo kubwa na zawadi mbalimbali kwa wateja watakao nunua bidhaa hizo kupitia WEBSITE ya JUMIA.

Katika biashara hiyo ya mtandaoni, Jumia Tanzania itashirikiana na wadau wake wakubwa kama Tigo na Tecno kwa ili kuwezesha kusogeza huduma kwa bei nafuu ambayo kila mtanzania ataweza kuimudu.

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa Jumia  mobile, Hilda Kinyunyu wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa katika mwezi huu watu wanaweza kuagiza simu kupitia mtandao wa Jumia na kupelekewa mahali popote walipo.

Kwa upande wa Tecno Mobilea itakua na duka maalumu katika mtandao wa Jumia ambapo simu za kampuni hiyo ikiwemo simu mpya maarufu ya Tecno Camon Cx itapatikna, pia Tecno Phantom 6, w5 na l9 plus. Mteja atakae oda simu za Tecno Mobile katika mtandao wa Jumia atapata zawadi mbalimbali zitakazomfikia pamoja na simu hiyo.

Wakenya, Wasomalia wafukuzwa tena Marekani
Singida Utd Wamnasa Mwingine Wakimataifa