Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa matukio ya uhalifu yamepungua Jijini Dar es salaam.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea na Operesheni kali ambapo mpaka sasa limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 152 kwa makosa mbalimbali ya kihalifu.

Ameyasema hayo mapema hii leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, Sirro ameongeza kuwa Operesheni ya kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali ni endelevu hivyo amewaomba raia wema kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo.

Aidha, katika hatua nyingine amesema kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu wawili wakiwa na vipande viwili vya meno ya tembo wakiwa katika harakati za kutafuta wateja wa nyara hizo za Serikali.

Hata hivyo, Sirro amekemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mikononi kwa kuwashambulia watuhumiwa badala yake waache kazi hizo zifanywe na vyombo husika kama Polisi

 

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 13, 2017
Video: Waziri Mwakyembe ajibu kwanini alihudhuria 'Press' ya Roma