Kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Keko Pharmaceutical Limited kilichopo Keko jijini Dar es salaam, kimepigwa faini ya shilingi milioni ishirini kwa kosa la kutiririsha maji taka kwenye makazi ya watu.

Hatua hiyo imefikiwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina alipofanya ziara ya kushtukiza ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda hicho.

Mpina amesema kufuatia uharibifu wa mazingira unaofanywa na kiwanda hicho wa kutiririsha maji taka kwenye makazi ya watu bila kutibiwa, na bila kuwa na kibali cha utiririshaji huo, amewatoza faini ya shilingi milioni ishirini inayopaswa kulipwa ndani ya wiki mbili.

Kwa upande wake Selemani Ndugwana, Meneja uthibiti na Ubora wa kiwanda hicho cha dawa alipokea adhabu hiyo, na kuomba kupunguziwa kwasababu ni kosa lao la kwanza.

Hata hivyo Mtendaji wa kata hiyo ya Keko, Samweli Magali amesema kuwa, kero ya uchafuzi wa mazingira kutoka kwenye kiwanda hicho cha madawa ni kubwa na hatari kwa afya za wakazi  wanaoishi jirani na kiwanda hicho.

 

Majaliwa ampa siku 18 Mkandarasi kukamilisha umeme Mlandizi
Kamanda Sirro amjibu Makonda