Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa operesheni ya kukamata watu wanaojihusisha na biashara ya shisha jijini Dares salaam inandelea kama kawaida na watuhumiwa wanashikiliwa na jeshi hilo.

“Watu wengi wanaojihusisha na biashara ya shisha wamekamatwa kwa mkoa wa Dar es salaam,na majalada yana andaliwa na mengine yamepelekwa kwa wakili wa Serikali kwaajili ya kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote”alisema Sirro,

Kamishna Sirro, amesema hayo baada ya kauli ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda aliyoitoa siku chache zilizopita ya kumtuhumu kuwa anashindwa kuwadhibiti wafanya biashara hao wanaojihusisha na shisha katika jiji la Dar es salaam.

Hata hivyo, Sirro ameongeza kuwa operesheni inaendelea kama kawaida ya kuwa kamata watengenezaji, wauzaji na watumiaji wa shisha,na amewaomba wananchi wa jiji la Dar es salaam, kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili liweze kudhibiti biashara hiyo.

Video: Kiwanda cha dawa za binadamu chapigwa faini Sh. Mil. 20
Ruge akimulika kipaji cha Ruby, aeleza anapomuona baada ya kuitosa THT