Mamlaka ya Serikali za mitaa, Wizara na Taasisi zote zimeagizwa kutoa taarifa za ajira zinazozalishwa kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kila robo mwaka.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu hoja ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye aliitaka Serikali itoe maagizo kwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri kutengeneza ajira angalau 20,000 kila mwaka katika miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri zao, na taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo iwe inatolewa kila mwaka kwenye Bunge la Bajeti.

“Napenda, kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015, Ibara ya 59 inazielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa zote nchini kuzingatia viashiria vya ukuzaji ajira katika mipango ya maendeleo ya ngazi husika pamoja na kutoa taarifa za mwenendo wa ajira kila robo mwaka,” amesema

.

Wakulima 2575 wanufaika na mkopo kutoka TADB
Askofu Banzi: Tuungane kupiga vita mtandao wa dawa za kulevya