Serikali imetakiwa kupiga vita dawa za kulevya ili kufikia azma ya kuwa nchi ya viwanda kwakuwa matumizi ya dawa hizo yanapoteza nguvu kazi nyingi ya taifa.

Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi wakati wa uzinduzi wa  Juma la Elimu lililofanyika Don Bosco Sekondari iliyopo Maweni Jijini Tanga.

Amesema kuwa ili kutimiza azma hiyo, ni lazima nchi iweke juhudi za kuteketeza mtandao wa dawa za kulevya hapa nchini ili vijana wengi watumikie taifa lao kwa nguvu zote.

“Kama tuanataka kuifanya nchi yetu kuwa ya viwanda, maana yake kila mmoja apate elimu ya madhara ya dawa za kulevya, lengo kubwa ikiwa ni kuondoa tatizo hili kwa vijana ambalo linapoteza nguvu kazi ambayo ingeweza kutumika katika shughuli mbalimbali,“amesema Askofu Banzi.

Aidha, ameongeza kuwa ni lazima kuwepo na mpango mkakati wa dhati wa kutokomeza mtandao huo ili kuweza kulinusuru taifa kuangamia na kuokoa maisha ya vijana.

Hata hivyo, Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Don Bosco, Gregory Mhuza  amesema kuwa wameamua kupanda miti katika Shule yao ili kuhakikisha mazingira yanakuwa katika hali ya usalama.

 

Video: Majaliwa aagiza taarifa za ajira kutolewa kila robo mwaka
Thomas Ulimwengu Kusota Benchi Kwa Miezi Mitatu