Wakulima 2575 wamenufaika na mkopo uliotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) baada ya kupata mkopo wa jumla ya shilingi bilioni 6.5 kwa vikundi 20 ili kuisaidia Serikali katika kujenga Tanzania ya viwanda.

Hayo yamesemwa mapema hii leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Francis Assenga wakati wa uwekaji saini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na Benki hiyo.

Assenga amesema Benki imeweza kuvisaidia vikundi vya wakulima wadogo wadogo 336 vyenye jumla wa wanachama 44,400 katika Mikoa ya Iringa, Morogoro na Tanga ili viweze kukopeshwa na Serikali pamoja na kutumia fedha hizo kwa ajili ya shughuli za kilimo na sio vinginevyo.

“Kupitia mafunzo haya TADB imewezesha jumla ya vikundi 19 kutimiza masharti na maandalizi ya msingi ya kuweza kukopa, Vikundi vingine vilivyobaki vinaendelea kupatiwa mafunzo ili viweze kufikia hali ya kuweza kukopesheka”, amesema Assenga.

Aidha, Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Rosebud Kurwijila amesema kuwa, Benki hiyo itatekeleza kwa vitendo juhudi za Serikali za Kujenga Uchumi wa Viwanda kwa kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Naye Msajili wa Hazina, Dkt. Oswald Mashindano amesema kuwa taasisi za umma zina wajibu wa kusaidia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali ili kuleta maendeleo endelevu nchini

Zlatan Ibrahimovic Amtega Jose Mourinho
Video: Majaliwa aagiza taarifa za ajira kutolewa kila robo mwaka