Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka nia ya dhati ya kupambana na dawa za kulevya na amewataka watendaji wote kuanzia ngazi ya vijiji wadhibiti suala hilo.

“Serikali haiwezi kuona vijana wanaangamia kwa dawa za kulevya. Tumeamua kudhibiti hali hiyo. Hii vita ni ya nchi nzima. Kuanzia sasa, viongozi wa Serikali za vijiji wakamateni wale wote wanaojihusisha na biashara hii.”

“Tunataka vijiji vyetu, kata zetu, wilaya zetu na mikoa yetu iwe safi bila hata chembe ya dawa za kulevya. Tukikuona kijana unayumbayumba au kuweweseka, tunakupima na tukikuta umetumia ile kitu, tunakukamata ili utuambie ni nani amekupa,” – Majaliwa

Video: Mpina atoa siku thelathini kwa Kampuni ya Red Sea kubomoa ukuta wake
Halmashauri Ilala kuweka utaratibu kuwalinda Bodaboda