Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amezindua wiki ya kinga tiba kwaajili ya kusaidia wananchi wa jiji la Dar es salaam. Makonda amesema kuwa kuna magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele kama vile Matende na Tezi dume ambayo husababishwa na mbu na hupelekea kupunguza nguvu kazi ya taifa. Amesema kuwa huduma ya kinga tiba imesambazwa katika kila sehemu ya mkoa wa Dar es salaam na kuwataka wale wanaobeza huduma hiyo kuacha kutoa taarifa zisizo na uhakika ambazo zinawachanganya wananchi , ameongeza kuwa kinga ni bora kuliko tiba hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kupatiwa huduma hiyo kwa gharama nafuu. Bofya hapa kutazama

Eric Bailly: Nitaimiss Man Utd Na Timu Ya Taifa Langu
Wanahabari Wa Ufaransa Wamkera Wakala Wa Marko Verratti