Wakala wa kiungo wa klabu bingwa nchini Ufaransa PSG,  Marco Verratti (Donato Di Campli) amekanusha uvumi wa mchezaji huyo kuwa mbioni kuuhama mji wa Paris.

Di Campli amesema taarifa ambazo zinaendelea kutolewa na baadhi ya vyombo vya habari vya mjini Paris kuhusu mchezaji wake kutakiwa na klabu za AC Milan na Juventus sio za kweli.

Amesema taarifa hizo zimepikwa kwa makusudi na baadhi ya watu wanaochukizwa na uwepo wa Verratti huko Parc des Princes, lakini ukweli ni kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 hana mpango huo.

“Kuna matumaini kwa Juve na Milan?” Donato Di Campli alihoji baada ya kuulizwa swali kuhusu tetesi za kuondoka kwa Marco Verratti.

“Marco anahitaji kushinda taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya akiwa na PSG, kwa sasa hakuna uwezekano wowote wa kuondoka.

“Jambo linalonikera mimi, ni vyombo vya habari vya Ufaransa kuendelea kukuza suala hili ambalo halina msingi, kwa sababu hakuna mantiki ya kuzunguzwa juu juu wakati wahusika ambao wanaweza kulijibu wapo”.

“Marco anastahili heshima.” Aliongeza Donato Di Campli

Verratti alijiunga na PSG mwaka 2012 akitokea nchini kwao Italia alipokua akiitumikia klabu ya Pescara.

Video: Makonda azindua wiki ya kinga tiba mkoa wa Dar es salaam
Pep Guardiola: Ningependa Kumtumia Yaya Dhidi Ya Man Utd