Bondia Manny Pacman Pacquiao jana ametangazwa rasmi kuwa miongoni mwa watu 12 walioshinda nafasi za useneta nchini Ufilipino.

Kutokana na ushindi huo, Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 amepata fursa ya kuweza kuwania nafasi ya juu zaidi nchini kwa siku za usoni.

Wachambuzi wa kisiasa nchini humo wameeleza kuwa katika uchaguzi wa rais utakaofanyika mwaka 2022, Pacquiao atakuwa na umri wa kutosha kikatiba kuwania nafasi ya Urais (katiba inataka umri wa miaka 40 na kuendelea), na kwamba kutokana na umaarufu wake mkubwa nchini humo anayo nafasi zaidi ya kushinda kiti hicho.

Bondia huyo alikuwa katika nafasi ya Ubunge kwa miaka miwili mfululizo (2013&2014), lakini alikuwa akikosolewa kutokana na kutumia muda mwingi katika masuala ya ubondia kuliko Ubunge.

Mwaka huu, Pacquiao alitangaza kustaafu masumbwi ili apate nafasi zaidi ya kuwatumikia wananchi wake wa Ufilipino akieleza kuwa dhamira yake ni kuhakikisha anawaletea maendeleo na kuboresha maisha yao.

Manispaa ya Kinondoni yamuwekea Manji kitanzi kingine ‘Coco Beach’
Wageni Watesa Ligi Ya Soka Marekani (MLS)