Mama Mjane, Benadetha Rwendela aliyekuwa amedhulumiwa Nyumba yake Plot No. 239 Block B Kunduchi Beach jijini Dar es salaam kwa kupigwa Mnada na Madalali kutoka Kampuni ya Nkanya Ltd kinyume na taratibu kisha kuamriwa kuondoka ndani ya siku 30 amemshukuru Makonda kwa kumsaidia kupata haki yake.

Akitoa shukrani zake amesema kuwa hakutarajia kuonana na mkuu huyo wa mkoa lakini baada ya kusikia habari zake za kudhulumiwa alimuita ofisini kwake na kumuunganisha na wanasheria wa mkoa kwa msaada zaidi wa kisheria.

“Namshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kanisaidia pakubwa sana, nilikuwa nahangaika sana, naipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kutujali wanyonge,”amesema Rwendela

Hata hivyo, Jana Makonda alitoa agizo la kusitisha mnada wa nyumba hiyo, huku akimuagiza Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa kuwakamata wote waliohusika na utapeli huo.

Video: Lowassa atoa maelezo mengine ziara ya Ikulu, Makonda awasha moto Dar es Salaam
Magazeti ya Tanzania leo Januari 16, 2018