Watu 11 wameiaga dunia na wengine 5 kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari hiace aina ya Nissan Caravan yenye namba za usajili T 542 DKE ambapo imegonga magari makubwa mawili ya mizigo.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo mida ya saa tano usiku wa kuamkia leo maeneo ya Mubigera Kata ya Nyantakara wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Ambapo amesema gari hilo dogo la abiria lilikuwa linatokea Kakonko Mkoani Kigoma kuelekea Kahama.

Kutokana na mwendokasi aliokuwa nao dereva huyo ambaye mpaka sasa hajatambuliwa jina lake aligonga magari mawili ya mizigo yenye namba za usajili T694 COX iliyokuwa ikivuta tela namba T 103 DKJ mali ya kampuni ya Mruruma Enterprises ya Dar es Salaam.

Aidha Ollomi amesema kuwa watu 9 wamefariki hapo hapo eneo la ajali, mmoja njiani akipelekwa hospitali na mwingine amepoteza maisha leo asubuhi na kuongeza kuwa 11 huku majeruhi 5 wanaendelea kupata matibabu katika hospitali teule ya wilaya Biharamulo.

Abiria waliokuwa katika gari dogo ni 17, kumi na mmoja wamefariki akiwemo dereva, watano wamejeruhiwa na mmoja yuko salama.

C1.jpeg

 

Video: Rais Dkt. Magufuli amewatikisa wazungu- Cyprian
Dkt. Mashinji awajibu wanaosema kiatu hakimtoshi