Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejipanga kuhakikisha kinarejesha Kata mbalimbali zilizochukuliwa na vyama vya upinzani katika jiji la Dar es Salaam na kusema kuwa kwa sasa wanajipanga kuhakikisha Kata pamoja na mitaa inarudi.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ubungo, Mbaruku Masudi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kwa sasa wameanza kuondoa changamoto mbalimbali ndani ya chama hicho kuhakikisha wanashinda na kukomboa mitaa na Kata ambazo zipo chini ya wapinzani.

“Tutahakikisha katika changuzi zozote zilizopo mbele yetu kama ule wa Saranga uchaguzi mdogo ni kuhakikisha tunarudisha mitaa iliyobaki na Kata zilizobakia,”amesema Masudi

Hata hivyo, katika uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika Novemba 26, 2017 uliwapa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Saranga Ubungo na kuweza kukomboa Kata hiyo ambayo awali ilikuwa chini ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Diamond, Harmonize, Jux na Vanessa wamfuta chozi Shilole kwenye harusi yake
Wolper afunguka pesa itayogharimu harusi yake