Leo Bungeni jijini Dodoma Serikali imetolea ufafanuzi suala la umiliki wa laini za simu zaidi ya moja, na kusema kuwa serikali inatamani kila mtanzania awe na laini moja kwa kila mtandao mmoja na ikitokea anahitaji kuwa na laini nyingine ya ziada afuate utaratibu maalumu utaomruhusu kumiliki laini hiyo.
Hoja hiyo imeibuliwa na Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ambaye aliuliza swali akisema.
”Mheshimwa Waziri amenukuliwa katika vyombo vya habari akisema kwamba kuanzia tarehe 1 may kutakuwa na usajili mpya wa laini zote kwa kutumia alama za vidole, ameendelea kwa kusema kwamba hakutakuwa na ruhusa ya kumiliki zaidi ya laini mbili mpaka ruhusa maalumu ya maandishi, Mheshimiwa unafahamu kuna maeneo mengine huduma ya aini nyigine hazipatikani hamuoni kwamba mtawatesa watu ambao huduma za laini nyingine hazipatikani” amehoji Selasini.
Tazama video ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akijibu swali hil la Selasini Mbunge wa Rombo
Aidha Serikali tayari imetoa tangazo kwa mitandao ya simu nchini kuanzia May 1 mwaka huu mitandao yote kuanza usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole huku ikimtaka kila mtazania kumiliki angalau laini moja kwa kila mtanadao.
;