Serikali kupitia, Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, uongezaji wa thamani na huduma za kifedha Vijijini (MIVARF), imetekeleza maombi 5 ambayo yanawasaidia wafugaji hao kuongeza thamani ya mifugo yao kupitia Soko la Kimkakati la mifugo Longido lililojengwa na Program hiyo.

Mwishoni mwa mwaka 2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira ,Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu ), Jenista Mhagama, alikuwa na ziara ya kukagua ujenzi wa soko hilo wilayani humo.

Aidha, baada ya ziara ya ukaguzi alikutana na wafanyabiashara ya mifugo, ambao waliwasilisha maombi 5, ambayo yangeweza kuongeza thamani ya Biashara za Mifugo na kutatua kero zote za wafanyabiashara wa mifugo wilayani humo.

Serikali ya awamu ya tano imeamua kuwasikiliza watu wanyonge na ambao wanajituma kuchapa kazi, lakini pia lengo la Program ya MIVARF ni kuongeza kipato kwa wananchi hasa waishio vijijini, kwa mantiki hiyo nilimuelekeza Mratibu wa Program Kutekeleza maombi yao haraka sana ili wafugaji hawa wapate tija ya ufugaji kupitia soko hili” amesema Mhagama

Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Mifugo wilayani Longido, Saruni Laizer amesema maombi waliyowasilisha serikalini ili waweze kupata tija ya mifugo kupitia soko la Kimkakati la Mifugo Longido yamefanyiwa kazi na Program ya MIVARF ndani ya miezi mitatu tangu wawasilishe,

Nyota wa Tenesi nchini Uingereza kuwania ubingwa wa Malkia
Kesi ya Nondo yasogezwa mbele, akana mashtaka yanayomkabili