Baada ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kusimama bungeni na kuomba mwongozo wa spika kuhusu kitendo cha kuvuliwa kofia ‘baraghashia’ na mbunge wa viti maalum CHADEMA Anatropia Theonest ikiwa ni siku tatu sasa, Naibu spika Dk. Ackson Tulia amesimama na kulizungumzia Bungeni  baada ya CCTV camera za bunge kuonyesha tukio hilo.

Nimepitia picha za video za siku hiyo na nimejiridhisha ni kweli baada ya kusomwa dua wabunge wa kambi ya upinzani walianza kutoka nje ya bunge na mbunge Anatropia alipita sehemu aliyokaa Goodluck na kumvua kofia aliyokuwa amevaa na kisha kutokanayo nje ya bunge” –Dk. Tulia Ackson

Naibu spika Dk. Ackson Tulia amesema pia :-

“Kitendo hicho kilikuwa cha kudharau kiti cha spika pia kilikuwa kitendo cha fujo ndani ya ukumbi wabunge, nachukua hatua ya kutoa onyo kali kwa mbunge Anatropia kwamba kitendo alichokifanyi ni ukiukwaji wa sheria za bunge na endapo atarudia sheria mahususi zitachukuliwa” –Dk. Tulia Ackson

Rais wa Equatorial Guinea amteua mwanae kuwa Makamu wa Rais
Rama Dee Adai ameolewa Australia, ajipanga kutoka na mdundo wa ‘Singeli’