Mkali wa RnB, Rama Dee amefunika kauli zilizokuwa zikitajwa na baadhi ya watu kuwa wasanii wa Bongo wanaozamia ughaibuni baada ya kupata ndoa huko wameolewa.

Rama Dee-2

Rama Dee akiwa na familia yake nchini Australia

Rama Dee ambaye ana mke ‘mzungu’ na mtoto alikiri kuwa yeye ameolewa nchini Australia na kwamba hurudi nyumbani kutembea na kufanya shughuli nyingine za kijamii.

“Ni kweli [nimeolewa Australia]… kwa sababu kwa kawaida kwa mila za Tanzania ukioa mwenzio anatoka kwao anakufuata, sasa mimi nimemfuata mwanamke Australia… iko hivyo,” Rama Dee aliiambia Friday Night Live ya East Africa TV na kuungwa mkono na Nay wa Mitego ambaye alimpongeza kwa kuwa mkweli.

Rama Dee amekuwa akikiri kuwa ‘mahaba’ ndio yaliyomfanya ahamie nchini Australia na sio kitu kingine.

Katika hatua nyingine, Rama Dee alitambulisha video yake ya kwanza ya ‘Kipenda Roho’ na kueleza kuwa ataendelea kutambulisha video nyingine za wimbo huo kwani amewaalika watayarishaji mbalimbali kufanya video kwa hisia zao kwa kadri wanavyoona inafaa n azote atazitambulisha.

Akizungumzia mpango wa kuwasaidia wasanii wanaochipukia nchini, alisema kuwa amekuwa akifanya mradi wa kuwatembelea wasanii wachanga hasa wale wa mitaani akijaribu kuwasaidia kuinuka. Alisema tayari ameshafanya ‘kitu’ kwa wasanii wa mitaa ya Kawe na maeneo mengine.

“Msichangae kusikia Rama Dee amepiga ‘RnB’ kwenye mdondo wa Singeli,” alisema.

Video: Tukio zima la Mbunge Goodluck kuvuliwa ‘baraghashia’ live - CCTV camera
Msajili wa vyama vya Siasa aitetea kauli ya Magufuli kuhusu Siasa