Wakazi wa jiji la Dar es salaam wameeleza kusikitishwa na ajali mbaya iliyotokea Mei 6 mwaka huu jijini Arusha, ambapo wanafunzi 33 na waalimu wawili pamoja dereva walipoteza maisha katika ajali hiyo.

Aidha wakazi wa jiji la Dar es salaam wametoa wito kwa madereva wa magari kufuata sheria za barabarani ili kuweza kuepukana na ajali hasa kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Hata hivyo, wakazi hao wamewataka wafiwa kuwa wavumilivu hasa kwa kipindi hiki kigumu cha majonzi hivyo kuwaomba wamtangulize mungu, kwani yeye ndiye muweza wa yote.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 10, 2017
Mvua kubwa zasababisha maafa jijini Arusha