Watu watano wa familia moja wamefariki dunia mkoani Arusha mara baada ya mvua kunyesha mfululizo kituambacho kilisababisha mafuriko makubwa kutokea na kusababisha maafa hayo

Maafa hayo yametokea katika Kijiji cha Kinyeresi wilayani Arumeru mkoani humo mara baada ya mti mkubwa kung’olewa na Mvua kisha kuangukia nyumba hiyo na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja .

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja waliofariki kuwa ni pamoja na Miliamu Jonathani(16), Grolia Jonathani (11), wengine ni pamoja na Giliad  Jonathani (31), Lazaro Lomnyaki
(26) na Best Jonathani (20).

Kamanda Mkumbo amesema kuwa mti huo uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji la Arusha.

Hata hivyo, ametoa wito kwa wakazi wa Arusha kuchukuwa tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na kuacha kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.

 

Video: Wakazi jijini Dar wazungumzia ajali ya wanafunzi iliyotokea Arusha
Video: Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watakiwa kuzingatia mipaka ya madaraka yao