Mwanaume mmoja nchini India amefanya tukio la aina yake baada ya kumsaka msituni nyoka mkubwa aina ya Cobra na kumuua kwa mikono mitupu akilipiza kifo cha mwanae wa kiume.

Katika kipande cha video kilichopata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube, mwanaume huyo anaonekana alikamata joka hilo kutoka kwenye mti na kulipiga chini mara kadhaa.

Mwanamme huyo ambaye anaonekana akiwa amevaa msuli pekee, alilikamata joka hilo mkiani na kulipiga chini bila kuhofia usalama wake kana kwamba alichokishika ni fimbo tu.

Taarifa zilizoripotiwa na gazeti la The Sun zimeeleza kuwa baadhi ya wanaharakati wa haki za wanyama wamepinga kitendo alichokifanya wakidai amemuua nyoka huyo kikatili!

Mchezaji Wa Timu Ya Taifa Ya Honduras Auawa
Mwanamke Ahukumiwa Kupigwa Mawe hadi Kufa