Damu ya mwanamke mmoja nchini Iran inatarajia kumwagika kwa kupigwa mawe hadi atakapokata pumzi yake ya mwisho baada ya mahakama nchini humo kumhukumu adhabu hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Iran wa LAHIG, mwanamke huyo ambaye ametajwa kwa jina moja la A.Kh, amehukumiwa adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika kupanga njama za mauaji ya mumewe.

Mahakama ya Iran ya Makosa ya Jinai iliyoko Rasht ambao ni mji mkuu wa jimbo la kaskazini la Gilan ndiyo iliyotoa hukumu hiyo ya kikatili jana ikiwa ni siku maalum ya ‘Haki za Binadamu’ ya umoja kimataifa.

Kiwango cha hukumu ya mauaji hakijashuka nchini Iran katika kipindi cha miaka michache iliyopita, kimeongezeka. Ingawa kupigwa mawe kumeendelea kupungua lakini majaji nchini humo wameendelea kutoa hukumu hiyo,” mwanaharakati wa haki za binadamu Iran aishie Toronto Canada, Maryma Nayeb Yazdi aliuambia mtandao wa FoxNews.

Video ya Mwanaume akimuua Kwa Mikono Mitupu Nyoka Mkubwa aliyemuua mwanae yapata Umaarufu, Iangalie Hapa
40 Waswekwa Rumande Sakata La Makontena