Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sitta alikuwa Spika wa kasi na viwango, Spika wa watu aliyependwa na kila mmoja kutokana na uadilifu wake wenye tija kwa Taifa.

Zitto amesema Marehemu Sitta alipopokea uongozi wa kuliongoza Bunge aliliboresha, aliwezesha kutunga kanuni mpya na kuliweka Bunge katika nafasi yake ya kikatiba pamoja na kuliunganisha Taifa.

Zitto amesema hayo leo Novemba 11, 2016 wakati wakuaga mwili wa Spika Mstaafu, Samweli Sitta bungeni mjini Dodoma ambapo kwa hisia kubwa alisema bado mwangwi wa sauti nene ya marehemu Sitta inasikika ikiwataka Mawaziri kujibu maswali kwa usahihi hali iliyoamsha hisia kubwa kwa wabunge na wananchi wote waliokuwa Bungeni hapo. Tazama video

Mahakama yampa dhamana Lema, Hatua ya Serikali yamrejesha
Wanafunzi vyuo vikuu waaswa kuepuka migomo na maandamano