Chama cha ACT Wazalendo kimetoa msimamo wake juu ya agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ambaye mnamo Julai 31, 2018 alimtaka kiongozi wa chama hicho na mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe kuripoti polisi mara baada ya kufanya mkutano wa hadhara na kuhutubia wananchi wa Kilwa mnamo Julai 29, 2018.
Ambapo Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema mawakili wa chama hicho wamesema matamshi ya Waziri Lugola hayana hoja ya msingi kisheria, hivyo amemtaka Zitto kuendelea na majukumu yake mpaka pale jeshi la polisi litakapo mtaka kuripoti kwani wito unaotolewa na polisi ni wito wa kisheria na wito unaotolewa na Waziri ni wito wa kisiasa.
Lakini pia Ado amesema hakuna sheria inayomzuia mbunge wa jimbo moja kumualika mbunge wa jimbo jingine kuhutubia katika mkutano wake ilimradi mkutano husika umefuata taratibu zote za kisheria katika kuitishwa kwake na hakuna sheria inayomzuia kiongozi wa chama cha siasa kuhutubia katika eneo lolote lile la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilmradi anazingatia sheria katika kufanyta hivyo.
Msikilize hapa chini.