Vigogo watatu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakabiliwa na kesi  ya kuomba rushwa ya dola za Marekani milioni nne sawa na zaidi ya shilingi bilioni nane za Tanzania.

Hayo yamesemwa na Wakili Mkuu wa Serikali , Mutalemwa Kishenyi  akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaaamna. Na kuwataja vigogo hao ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA, Epharaim Mgawe,  Mkurugenzi wa Uhandisi TPA, Bakari Kilo, Meneja Manunuzi TPA Theophil Kimaro, na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya DB Shapriya Ltd Kishor Shapriya.

Aidha, Wakili Kishenyi amesema washtakiwa hao wadaiwa kati ya mwaka 2009 na 2012 mahali pasipojulikana wakiwa katika nyadhifa zao kupitia Wakala wa Kampuni ya DB shapriya Ltd waliomba rushwa ya dola za Marekani milioni nne kama kishawishi cha kuiwezesha kampuni hiyo kushinda zabuni yenye namba AE/0116/2008-2009/10/59 kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta TPA katika RAS ya Mji Mwema.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa walikana kuhusika na kutenda makosa hayo. Wakili Kishenyi alisema upelelezi wa kesi bado unaendelea, pia hawana pingamizi la dhamana endapo washtakiwa watatimiza masharti ya dhamana yatakayotolewa na mahakama.

Vigogo hao waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowataka kuwa na wadhamini wawili waaminifu watakaosaini hati ya dhamana ya Sh milioni 500 kwa kila mmoja.

Walioiba gari la Afisa wa JWTZ na mwanae wakiona 'cha mtemakuni'
Yanga Yaboresha Safu Ya Utendaji