Serikali imesema kuwa imedhamiria kuhakikisha wananchi wote wakiwemo wa wilaya ya Nachingwea wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao, hivyo wametakiwa kuendelea kuiamini.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namatula ‘A’ na kijiji cha Mtua ambao waliosimamisha msafara wakati akielekea Kata ya Kilimarondo wilayani Nachingwea.
“Serikaliya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini vikiwemo vijiji vya wilaya ya Nachingwea ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo.”amesema Majaliwa
Amesema kuwa Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.
Hata hivyo, ameongeza kuwa mbali na huduma ya maji, pia Serikali imedhamiria kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).
- Waziri Mkuu akutana na makamu mwenyekiti wa bunge la China
-
Serikali yawatahadharisha Wahasibu
-
Video: Makonda afanya ziara mkoani Morogoro