Baraza la Viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya Tanzania, limeunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, za kupambana na watu mbalimbali wanaotuhumiwa kujihusisha na utumiaji pamoja na uuzaji wa dawa za kulevya.
Baraza hilo limeiomba serikali  kumuongezea ulinzi Makonda  kwa kuthubutu kutaja watu wanaojihusisha kwa namna moja au nyingine na dawa hizo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum ,ambapo amesema kuwa Makonda anapaswa kuongezewa ulinzi kutokana na ujasiri alio nao wa kuthubutu kuwataja kwa majina watu hao.
“Sisi kama baraza tunapiga vita na kulaani hatua yoyote ya kushiriki katika biashara au utumiaji wa dawa za kulevya, kwa kuwa matumizi ya dawa hizo yamekuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika nchi yetu na yanapotokea nguvu kazi ya Taifa kwa vile wahanga wakubwa wa matumizi ya dawa hizi ni vijana,”amesema Sheikh Salum.
Amesema kutokana na ugumu wa kazi hiyo aliyoianzisha baraza hilo linamuombea kwa mwenyezi mungu ili ampe ulinzi wake na kinga yake, na azidi kumpa moyo wa ujasiri wa kupambana na maovu yote yanayo haribu sifa ya Taifa na vijana kwa ujumla.
Aidha, Salum amesema kwa hivi sasa Makonda ameshanza kutengenezewa majungu, fitina na uzushi mbalimbali ili kumkatisha tamaa na aonekane mbaya kwa watanzania lakini hawatafanikiwa endapo atamtanguliza mwenyezi mungu katika mapambano hayo.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa baraza hilo ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wengine waige mfano wa Makonda wa kupambana na uovu huo mkubwa ambao ni janga kwa Taifa kwani Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana

Tundu Lissu akiri alichokisema
Mbarawa ateua timu ujenzi terminal III, atumbua mmoja