Majanga mengi yanayoikumba dunia hivi sasa, yanachochea kuongeza nia ya kufanikisha malengo hayo ifikapo mwaka 2030 itakayoshirikisha wadau na viongozi wa ulimwengu na kupata matokeo chanya katika kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya ya tabia nchi, vita na kutokuaminiana.

Hayo, yamebainishwa hii leo Septemba 20, 2022 jijini New York nchini Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres wakati akihutubia viongozi wa nchi na vijana katika mkutano wa kutathmini mwelekeo wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Ameyataja miongoni mwa majanga hayo mbali na vita, mabadiliko ya tabianchi, kutoweka kwa kuaminiana, mengine ni mizozo, mgawanyiko, umaskini, ukosefu wa usawa, ongezeko la gharama za maisha, kupanda kwa bei ya chakula na nishati huku vipato vinaporomoka na ukosefu wa ajira.

Mwandishi, Nargiz Shekinskaya wa UN News, akimhoji Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres. Picha na UN /Mark Garten.

Amesema, “Kila janga linarudisha nyuma SDGs na katika mazingira kama hayo, inashawishi kuweka kando vipaumbele vyetu vya maendeleo, visubiri siku njema lakini maendeleo hayawezi kusubiri.”

Katibu Mkuu, pia amesisitiza kuwa elimu ya watoto haiwezi kusubiri ajira zenye stahai, usawa kwa wanawake na watoto wa kike halikadhalika na afya bora, huku akisema hatua sahihi kwa tabianchi navyo haviwezi kuwekwa kando visubiri kesho isipokuwa wakati ni sasa wa kufanikisha malengo husika.

Guterres ameongeza kuwa, “Nyote mlio hapa na wengine mnaofuatilia mkutano huu kwa njia mbalimbali kutoka pande mbalimbali za dunia, mnanipatia matumaini makubwa kwamba tunaweza kuweka mikono yetu kwenye gurudumu la maendeleo na kulisongesha mwelekeo mpya.”

Serikali: Makusanyo ya tozo yamesaidia huduma za Msingi
Al Hilal yamuumiza kichwa Nassredine Nabi