Katika sehemu ya kwanza la makala hii tuliona kuwa Bara la Afrika linajulikana ulimwenguni kwa sifa nyingi ikiwemo utajiri wa rasilimali, umaskini, ukosefu wa usalama na ufisadi na sehemu hiyo ya kwanza tulimuangalia muasisi wa Taifa la Afrika ya Kusini, Hayati Nelson Mandela.
Baadaye katika sehemu ya pili tukamuona Mkongwe Haile Selassie, mtawala wa Ethiopia kuanzia 1916 hadi 1974, kisha sehemu ya tatu moja tukamuona Kwame Nkrumah, Rais wa kwanza mzawa wa Ghana na mwanzilishi wa Taifa la Ghana, akiwa ni mwana-Pan-Africanist ambaye alianzisha Umoja wa Afrika – AU, ambao zamani ulijulikana kama Umoja wa Umoja wa Afrika – OAU.
Aidha, tuliona jinsi ambavyo hakuridhika na uhuru wa nchi yake pekee, akisema uhuru wa Ghana hautakuwa na maana kama nchi zingine za Kiafrika zitaendelea kuwa chini ya Utawala wa Kikoloni na hii ikaoneonesha jinsi mwanaharakati huyu alivyokuwa tayari kujitoa muhanga kwa ukombozi wa Bara zima la Afrika.
Sehemu ya nne tulimuangazia Baba Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuona jinsi muasisi huyu wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea na jinsi jina lake la mwalimu lilivyopatikana. akiwa ni kati ya viongozi wachache wa Afrika, ambao wameacha madaraka kwa hiyari baada ya kutawala kwa muda mrefu.
Leo tunaingia sehemu yetu tatano ambapo tunakumuka kwamba Januari 17, 1961, kiongozi wa harakati za uhuru na aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza kuchaguliwa kisiasa wa Kongo DRC, Patrice Émery Lumumba, aliuawa akiwa na miaka 36 baada ya kukamatwa kufungwa kamba, kupigwa kikatili (pamoja na mawaziri 2) kwa kile kinachoonekana kuwa ulikuwa ni ushirikiano wa Marekani na Ubelgiji.
Lumumba alikuwa kiongozi pendwa wa wananchi wakati wa harakati za uhuru mpaka uhuru, huku akiwa na lengo la kuiondoa Kongo kwenye ukoloni mamboleo wa Ubelgiji, kitendo ambacho serikali ya Ubelgiji haikufurahishwa nacho.
Hali hiyo, ilipelekea Wakoloni hao kutafuta kila mbinu za kumuangamiza na kufanikiwa, huku wakitumia mgongo wa kundi la wapiganaji wa Mobutu Seseseko na alikuwa ni Kiongozi wa kwanza wa kuchaguliwa nchini Kongo, huku akiacha alama kubwa kwa nchi hiyo na Afrika kiujumla, na baadhi ya watu wakimuita ndiye ‘Che Guavara’ wa Afrika.
Lumumba ni nani?
Lumumba alikuwa Mwanamapindunzi ambaye Afrika ilimuitaji sana, Mabeberu walilitambua hilo na kuhakikisha wanamfutilia mbali. Sijui kama Afrika ya sasa tunamuenzi Patrice Lumumba.
Alitamani na kupigania Afrika iwe uhuru na tena si yenye uhuru bandi bali uhuru kamili wa kujitawala KISIASA, KIUCHUMI na KIUTAMADUNI pia Alitamani kuona rasilimali zilizopo Afrika zinatunufaisha sisi Waafrika wenyewe.
Sijui kama tunao vijana katika Afrika ya sasa kama Patrice Lumumba, na awali ya yote ngoja nikupe baadhi ya kauli zake alipata kuzitoa kipindi yupo Duniani, “Msinililie, wazalendo wenzangu, najua kuwa nchi yangu, inayoumia sana hivi sasa, itaweza kulinda Uhuru wake. Idumu Kongo! Idumu Afrika.”
Nukuu za Lumumba.
“Hakuna mateso wala vitendo vyovyote vya kinyama vitakavyonifanya kuomba huruma, ni bora kufa kwa heshima, nikiamini kabisa na kujiamini kuhusu hatma ya nchi yangu kuliko kuishi kwenye utumwa na kuvunja misingi yangu.
“Ipo siku historia itasema, sio historia iliyoandikwa Umoja wa Mataifa, Washington, Paris au Brussels, lakini historia itakayofundishwa katika nchi zilizoondoa ukoloni na vibaraka wake. Afrika itaandika historia yake iliyojaa utuna heshima.”
Barua ya Lumumba kwa Mkewe.
Patrice Lumumba alimwandikia barua mkewe Pauline akiwa gerezani kumjulia hali na kumjulisha mambo mengi kabla ya kifo chake. Tunaambiwa katika historia Januari 17, 1961 Patrice Lumumba aliuwawa kwa kupigwa risasi na kuzikwa kusikokujikana mkewe pia naye alikamatwa na kuvuliwa nguo kisha kuzungushwa mitaani na kisha baadaye kuuawa.
Lakini Patrice Lumumba alikua mwanaume wa shoka na jasiri ikisemekana kuwa wazungu waliogopa hata maiti yake kwani walimuunguza kwa tindikali. Alikuwa ni mwanasiasa mwanamapinduzi wa Kongo ambaye baadaye alikua Waziri Mkuu wa kwanza wa taifa hilo kuanzia Julai hadi Septemba 1960.
Nkrumah wa Ghana, Julius Nyerere wa Tanzania, Abdurahman Babu wa Zanzibar, Tom Mboya wa Kenya, Kanyama Chiume wa NyasaLand na Ahmed Sekou Toure wa Guinea hawa wote walimutambua Patrice Lumumba na mchango wake kwa Kongo na Bara Afrika kwa ujumla.
Alikuwa raia wa Ubelgiji ambaye pia alikuwa rais wa chama cha wafanyakazi cha Kongo na baada ya kurejea Kongo, Lumumba alianzisha Vuguvugu la Kitaifa la Kongo (MNC) na kutumia itikadi za Pan-African kushinikiza uhuru wa nchi yake.
Juhudi zake zilituzwa kwani Kongo, ambayo sasa inajulikana kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikawa taifa huru mnamo Juni 30, 1961 na aliheshimiwa sana kwa utu wake mkubwa na ustadi wa mawasiliano.
Cha kusikitisha ni kwamba uongozi wake wote haukuwa wa muda mrefu kwani alitimuliwa madarakani na Kanali Joseph-Desire Mobutu, akajitwalia cheo cha Mobutu Sese Seko Nkuku wa Banga, na baadaye kuuawa Januari 1961 akiwa na umri wa miaka 35 tu wakati wa ukatili wake.
Ripoti ya mwaka 2001 ya Tume ya Ubelgiji iliyomhusisha moja kwa moja Rais Eisenhower) pia ikumbukwe kwamba hii ilikuwa siku 3 kabla ya kuapishwa kwa JF Kennedy (tarehe 20) na JFK haikufahamishwa chochote hadi tarehe 13 Feb.
Mzozo wa Madini.
Inaarifiwa kuwa, asilimia 80 ya uranium iliyotumika katika mabomu ya Hiroshima na Nagasaki ilitoka kwenye mgodi wa Shinkolobwe (tazama picha) katika BelgianCongo wakati huo. Katika miaka ya 1940 na 1950, Kongo ilikuwa muuzaji nambari moja wa uranium kwa Marekani.
Wakati Ujerumani ilipoiteka Ubelgiji mnamo Juni 1940, Marekani iliishawishi kampuni ya Ubelgiji iliyosimamia Shinkolobwe kuhamisha madini yake yote ya uranium hadi Marekani kwa uhifadhi. Tani mia mbili za madini zilisafirishwa kutoka Kongo hadi Staten Island, NY, na kuhifadhiwa huko.
Wakati Mradi wa Manhattan ulipozinduliwa mwaka wa 1942, serikali ya Marekani hatimaye ilinunua tani 1200 za uranium iliyokuwa imekaa New York, pamoja na tani 950 ambazo bado zimekaa Kongo.
Ili kupata hizo tani 950 zijazwe na kusafirishwa, waangalizi wa Ubelgiji waliendesha zamu usiku na mchana, ambapo wachimba migodi walipanga na kufungasha urani kwa mikono kwa muda wa majuma mawili hivi moja kwa moja.
Inawezekana wachimbaji waliwekwa wazi kwa mionzi ya thamani ya mwaka katika kipindi cha wiki hizo, na wanaweza kuwa hawakuwa na wazo la hatari ya kazi yao – lakini hiyo ni hadithi ya siku nyingine.
Wamarekani wahusishwa.
Katika miaka ya 1950, Marekani ilitaka kuhodhi sekta ya uranium nchini Kongo ili kuzuia Umoja wa Kisovieti kupata ufikiaji. Kwa hiyo, Marekani ilificha kiasi cha uranium walichokuwa wakichimba kutoka kwenye migodi ya Kongo na kufidia gharama za wachimbaji hao ambao waliendelea kulipwa ujira mdogo na kuzidiwa kazi.
Wakati Kongo ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1960, Lumumba akawa waziri mkuu wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia wa nchi hiyo mpya. Lumumba aliweka wazi kuwa hataipa Marekani kiasi cha uhuru sawa na Ubelgiji iliyokuwa nayo wakati inadhibiti Kongo, akiitia wasiwasi serikali ya Marekani.
Jimbo la Katanga lajitenga
Siku 11 baada ya DRC kupata uhuru, jimbo la Katanga ulikokuwa na mgodi wa Shinkolobwe likajitenga na nchi hiyo. Kampuni za uchimbaji madini za kibinafsi zinazofanya kazi na serikali za Magharibi zikafikiria uwezekano wa kupanga kujitenga, ili kupata uzalishaji wa urani bila kujali ni nani aliyeingia madarakani.
Baada ya kujitenga, Lumumba aliufikia Umoja wa Kisovieti na majimbo mengine kwa msaada, ambayo ilizidisha wasiwasi wa Amerika. Baada ya chini ya miezi 6 madarakani, Lumumba aliuawa katika misheni iliyoidhinishwa na Rais wa Marekani Eisenhower.
Mobutu aingia Madarakani
Kwa msaada wa CIA, Mobutu aliteuliwa kuwa kiongozi mpya wa DRC…Mobutu alidhibiti uchimbaji wote wa madini kutoka mkoa wa Katanga na sote tunajua historia ya DRChuku ikisisimua mwili ukiangalia hawa wapigania uhuru wa kizazi hicho walivyokuwa wanashirikiana kumng’oa MKOLONI Barani hapa kwa mtindo hasi.
Neno la Mwisho la Lumumba
“Tumezoea dhihaka na matusi, tumepigwa asubuhi mchana na usiku, kwa sababu sisi ni watu weusi. Tumeona ardhi yetu ikinajisiwa. Tumeona sheria zikitambua wenye nguvu na sheria tofauti kati ya watu weusi na watu weupe. Hatutasahau mamlaka zikijaza watu kwenye jela, watu ambao hawakukubali kwamba haki ni ukandamizaji na unyonyaji” – Patrice Lumumba.
Juni 30, 2022 Congo iliingia katika historia ambapo ilifanyika shughuli za maziko ya mabaki ya Waziri Mkuu huyo wa kwanza na Kiongozi wa uhuru wa nchi hiyo ambapo Mabaki hayo ni jino la Patrice Lumumba.
Mara baada ya kuuawa, mwili wa Hayati Patrice Lumumba uliyeyushwa kwenye tindikali (Acid) na kisha baada ya hapo Afisa mmoja wa Polisi wa Ubelgiji aliamua kulihifadhi jino la Hayati Lumumba na hatimaye likarejeshwa nchini Congo na kukabidhiwa kwa familia ya Lumumba kwenye hafla iliyofanyika Brussels.
Mabaki hayo yaliwekwa kwenye jeneza lililofunikwa kwa bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC na kisha kuzungushwa maeneo kadhaa ya nchi hiyo, ili kuwapa watu nafsi ya kutoa heshima zao kwani haikufahamika alizikwa wapi awali.
Enzi za uhai wake, Patrice Lumumba aliwahi kusema tatizo kubwa la Afrika ni kwamba wenye akili hawana madaraka, na wenye madaraka hawana akili (The problem with Africa is that those with ideas have no power and those with power have no ideas).