Serikali ya Korea Kusini imefichua siri kubwa ya nchi hiyo kuwa serikali ina mipango ya kuharibu, Kushambulia na kuangamiza kabisa mji mkuu wa Korea kaskazini, iwapo ishara  yoyote itajitokeza kuwa kuna mipango ya kushambuliwa kwa nukilia.

Shirika la Habari la Yonhap lililo na uhusiano mkubwa na Korea Kusini limesema kuwa  wabunge nchini humo wamepewa mpango huo. Mpango huo unanuia kuharibu kabisa makombora yote yenye zana hatari kukiwemo nyukilia.

Taarifa hii imetoka siku mbili baada ya Korea Kaskazini kulipua angani jaribio kubwa zaidi la kinyukilia, ambalo limetoa dhana kuwa Korea Kaskazini imepiga hatua kubwa katika utengenezaji wa zana za kinyukilia

Ndesamburo adai jahazi la nchi linazama, Ole Sendeka ajibu mapigo
Marekani Yaadhimisha Shambulio La Septemba 11