Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliokuwa umepangwa kufanyika leo katika ukumbi wa Karimjee umeingia dosari baada ya kuzuka vurugu kubwa zilizoanzishwa na madiwani wa vyama vinavyounda Ukawa, waliopinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo.

John Mnyika

Madiwani hao wa Ukawa waliokuwa wamejiandaa kuanza kufanya uchaguzi huo, walipinga tangazo la Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuahirisha uchaguzi huo akidai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepeleka pingamizi Mahakamani.

Vurugu2

Ukawa walipinga kwa nguvu tangazo hilo na kubaki ukumbini wakitaka waendelee kupinga kura kwani akidi ilikuwa inatimia na kwamba hawakupata barua yoyote ya awali kuhusu pingamizi hilo.

Vurugu3

Hata hivyo, Polisi zaidi takribani 15 waliingia ukumbini na kuwataka madiwani hao kutii tangazo la Mkurugenzi na kuondoka ukumbini. Uamuzi huo wa Polisi ulizua varangati ukumbini humo na hali ya utulivu ilivunjika kabla ya kurejea baadae.

Ali Kiba aandaa kitu na R-Kelly
TANESCO yawasilisha maombi kupandisha bei ya umeme